Sifanyi tena u-video queen, mimi ni Msanii-: Amber Lulu

  Share this

  Mmoja kati ya warembo ambao wamejipatia umaarufu mkubwa sana kupitia video za muziki hapa Bongo ni pamoja na Amber Lulu, mrembo ambaye mikogo yake inazidi kumuweka kwenye ramani kila kukicha.

  Amber lulu

  Kitu ambacho kiliweza kumfanya kufahamika zaidi na hadi baadaye kuamua kuhamia upande wa pili wa shilingi na kuanza kuimba, na haikuwa ngumu sana kwake, kutokana na ngoma yake ya kwanza kuweza kupokelewa vizuri kitaani.

  Amber Lulu ametusanua kwamba hivi sasa amekwisha kuachana na mbanga za kufanya u-video queen kwenye video za muziki hapa Bongo na badala yake ameamua kufungua kampuni yake ambayo itakuwa inasimamia ma-video queen.

  Akibonga na Perfect255, Amber Lulu ametusanua kuwa hivi sasa yeye ni msanii na hawezi kurudi nyuma, badala ya yeye kuitwa kama video queen, hivi sasa yeye ndio anatakiwa kuwaita hao ma-video queen ili washiriki kwenye video zake.

  “Mimi sifanyi hivyo vitu tena, mimi sasa hivi ni msanii, kwahiyo siwezi kurudi nyuma, mimi sasa hivi natakiwa niwaite ma-video queen ambao watakuwa kwenye ngoma zangu, me ni boss wa ma video queen na soon nafungua kampuni yangu ambayo itakuwa na ma-video queen 10 wakali.” Alisema Amber Lulu.

  Kirefu zaidi unaweza kumsikiliza Amber Lulu kwa kubonyeza kitufe cha play kwenye video hii hapa chini.

  Dondosha comments


  Share this