SIMULIZI: SINA KOSA (SEHEMU YA KWANZA)

  Share this

  Sina kosa ni simulizi nzuri ya kufundisha, kusisimua na kuelimisha ambayo itakuwa inaruka kila jumatatu, jumatano, ijumaa na jumapili….

   

  Kuwa karibu nasi ufurahie na ujifunze, usisahau kushare na kuacha comment yako…. Karibu

   

  “kaka mbona unanikanyaga jamani, inamaana huoni kweli au makusudi tu jamani”
  Ilikua ni sauti ya msichana akilalamika ndani ya daladala.
  “we dada vipi, kwani ulitakaje sasa, kazi kujilalamisha tu, usipotaka kukanyawa nunua gari yako binafsi sio kudandia daladala basi”, sauti ya kiume ilijibu tena ilijibu kwakujiamini sana kiasi kwamba kila mtu ndani ya daladala ile alishangaa sana kiasi kwamba kuna waluothubutu kuingilia mabishano yale, lakini kijana Yale hakuonesha kujali lolote lililoendelea katika daladala ile.

   

  Kituo kilichofuata kijana Yule alishuka tena alishuka peke yake hakuna mtu mwingine aliyeshuka katika kituo kile, watu walizidi kumshangaa kijana Yule asiyekua na maadili hata kidogo.

  Watu walimgeukia binti yule ambaye aliitwa Evah na kumpa pole kuhusu yaliyomsibu na wengine walisema msamehe kwani hajui alilofanya na wengine walisema”vijana wa siku hizi pindi wakoseapo hawajui omba radhi msamehe bure”, Evah aliitikia kwakutikisa kichwa kuonesha kukubaliana na watu hao.

  Konda aliyekua kimya kwa kipindi kirefu bila ya kuongea chochote akasema”pole sana dada yangu msamehe tu lakini mmmmmh”, konda aliguna bila yakusema kitu, mama mmoja aliuliza “mbona mmh konda, kuna nini tena?,

  konda alisita kisha akasema”nina wasiwasi na kiumbe kile uenda si kumbe wa kawaida maana miguu yake alipokua akishuka kama kwato si kwato”,
  Kwato!!!!!!, walisema kwa pamoja watu waliokua ndani ya daladala kisha konda akajibu,
  ” ndiyo, lakini tuachane na hayo labda sijaona vizuri jamani”, konda alimaliza na kuwaachia maswali mengi abiria.

  Je nini kitafuata katika sehemu ya pili, tukutane jumatatu mida na majira kama haya.

  Dondosha comments


  Share this