Sina vita na mtandao wowote wa kuuza nyimbo-: Diamond Platnumz

  Share this

  Tangu Diamond Platnumz azindue mtandao wake wa kuuza nyimbo online (Wasafi.Com) kitaani kumekuwa na story kuwa Diamond hana maelewano mazuri na mitandao mingine ya kuuza ngoma online.

  Perfect255 imemtafuta Diamond Platnumz na kupiga nae story kuhusu ukweli juu ya tetesi hizo.

  “Me sijawahi kuwa na vita na mtandao wowote wa kuuza nyimbo, kwasababu kama wasafi.com imekaa pale kwa nia njema tu. Wasafi.Com tumekuja kitofauti na mitandao mingine kuanzia kwenye uuzaji wa nyimbo hadi kwenye ulipaji wa wasanii, lengo ni kukuza industry, kwahiyo mtu ambaye anaichukia wasafi.com basi yeye hataki sanaa iendelee, labda ana maslahi yake yeye binafsi ambayo hayawafaidishi wasanii.” Alisema Diamond.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumsikiliza Diamond Platnumz akifunguka juu ya issue hiyo intro to outro.


   

  Dondosha comments


  Share this