SIpendi Tiffah awe msanii, watamla sana!-: Diamond Platnumz

  Share this

  Juzi kati msanii Diamond Platnumz alikuwa jijini Nairobi katika media tour ikiwa ni pamoja na kumtambulisha msanii wake mpya ambaye amemsaini kwenye lebo yake ya WCB Wasafi anayefahamika kwa jina la Lavalava.

  Na moja kati ya media ambazo alifanya nazo interview ni pamoja na NTV ambapo DIamond alitisha kwenye kipindi cha The Trend.

  Diamond Platnumz aliulizwa maswali mengi ila moja kati ya hayo ni pamoja na angependa watoto wake wawe watu wa aina gani. Ndipo Diamond alipofunguka kuwa angependa mwanaye wa kiume ambaye ni Nillan awe msanii kama yeye baba yake ila kwa upande wa mwanaye wa kike ambaye ni Tiffah hapendi kabisa awe msanii kwasababu anahisi atatumika sana.

  “Napenda mwanangu wa kiume awe msanii kama mimi baba yake! Ila sipendi mwanangu wa kike awe msanii! Kwasababu Watamla sana!” Alisema Diamond Platnumz.

  Unaweza kuisikiliza kwa ufupi interview hiyo ambayo alifanyiwa Diamond Platnumz na kituo cha NTV cha nchini Kenya kwa kubonyeza kitufe cha play kwenye video hii hapa chini.

  Dondosha comments


  Share this