Sitambui U-Boss wa Alikiba kwenye Lebo ya Rockstar-: Baraka Da Prince

  Share this

  Siku chache zilizopita lebo ya muziki ya Rockstar 4000 ilimtambulisha mkali wa muziki nchini Alikiba kama mmoja wa viongozi katika body ya madirector katika lebo hiyo.

  Alikiba na Viongozi wenzie Rockstar 4000

  Ila jana usiku kwenye kipindi cha Ala za Roho ya Clouds fm Diva The Bawse alikuwa na Exclusive interview na Baraka Da Prince ambaye naye pia ni msanii kutoka chini ya uongozi wa Record Label hiyo.

  Cha kushangaza ni pale Baraka Da Prince alipo kanusha kuzifahamu taarifa za Alikiba kupewa uongozi katika lebo hiyo na kudai kuwa hata yeye anaziona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii tu.

  Baraka Da Prince amedai kuwa bado hajapewa taarifa kutoka katika uongozi wa juu kuwa Alikiba ni mmoja wa viongozi katika lebo hiyo, na hivyo hamtambui Alikiba kama kiongozi katika lebo hiyo.

  Unaweza kuona ni kipi kinaendelea baina ya wakali hawa ikiwa hivi karibuni kumekuwa na story zinazo wahusisha kutokuwa na maelewano mazuri. Niachie comment yako kwa chochote ambacho umekielewa kuhusu wakali hawa.


   

  Dondosha comments


  Share this