Sitegemei kuwa chini ya WCB wala Rockstar, napambana mwenyewe!-: Aslay

  Share this

  Ikiwa WCB na Rockstar zinatambulika kama lebo kubwa za muziki hapa nchini na ndoto za wasanii wengi wachanga na wakubwa ni pengine kuwa chini ya lebo hizo na kazi zao kuweza kusimamiwa hapo kwa nguvu kubwa.

  Ikiwa ni wiki chache tu baada ya kuripotiwa taarifa za waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band kila mmoja kuanza kufanya kazi kama solo artist na tetesi za chini ya carpet kudai kuwa Maromboso ambaye ni mmoja kutoka Yamoto Band kutangazwa kusaini wa na WCB wakati wowote, Aslay amekuwa na mtazamo tofauti.

  Akipiga story na Perfect255, Aslay amefunguka kuwa hana mpango wa kuwa chini ya lebo kama Wasafi wala Rockstar kutokana na kuwa malengo yake ni kuweza kufika mbali zaidi hata ya level hiyo na hadhani kama akiwa chini ya lebo hizo lengo lake litatimia.

  “Sitegemei kusainiwa WCB wala lebo nyingine yoyote kutookana na mimi kama mimi nina ndoto za kufika sehemu kama aliyofika Chibu ama aliyofika Alikiba, kwahiyo itabibi nikaze mimi kama mimi ili niweze kuhakikisha nafika mbali zaidi.” Alisema Aslay.

  Bonyeza play uweze kumsikiliza Aslay akitema cheche kuhusiana na mchongo huo.


   

  Dondosha comments


  Share this