style za kucheza mziki zilizotikisa nigeria

  Share this

  Leo nimeona sio mbaya nikikusogezea style za kucheza mziki ambazo kwa hakika zilitikisa na bado nyingine zinatikisa nchini Nigeria.

  baadhi ya style hizo zimeanzia nchini Nigeria na nyingine zimetokea nje ya Nigeria ila kutokea kuwa na mvuto zaidi kwa wasanii wa muziki pamoja na mshabiki nchini Nigeria pamoja na Africa kwa ujumla

  MAKOSSA– Ni miongoni mwa style ya kucheza mziki ambayo hasa chimbuko lake imetokea kwa msanii awilo longomba wa congo, style hii kucheza ni vyepesi na unachotakiwa kufanya ni kutikisa kiuno huku ukicheza vizuri na mapigo ya beat.

  GALALA– ni style ambayo ilitumiwa na bado inatumiwa katika kusheherekea ubingwa, style hii hasa hutumika pale mtu unapokuwa nafuraha mfano kupata kazi, kufahuru mtihani, hivyo lkatika matukio hayo ya furaha style ya galala ndiyo hutumika.

  MOONWALK– style hii ni miongoni mwa style za mfalme wa pop marehemu “Michael Jackson” ambayo ilikuwa ikichezwa kwa kupeleka miguu nyuma na kuirudisha mbele vile vile kwa wakati mmoja.

  ALANTA– style hii ikiwa ni chimbuko la style za Nigeria huchezwa kwa kuweka mikono chini na kisha kushika mguu mmoja juu. style hii nchini Nigeria ni maarufu na huchwa na wanafunzi, wafanyakazi na hata waanzilishi wa makampuni.

  SHAKITI BOBO– ni miongoni mwa style maarufu nchini Nigeria ambayo imeanzishwa mwaka 2015 na ikumbukwe kuwa ni style iliyoomvutia msanii Ciara wa marekani kipindi alipokuja Nigeria na baada ya kuona style hiyo ikichezwa akaombwa kufundishwa.

  SHOKI– style ambayo imevuka mipaka sio afrika tu ila hata nchi za ulaya, wengi wanasema style hii ilikuja baada ya kuona vile “ombaomba” wanavyoomba msaada.

  YAHOOZEE– ni style inayochezwa na vijana wakisasa nchini Nigeria katika kumbi za mziki, inaaminika chanzo cha style ilikuja kwa namna vile vijana watumiaji wa mtandao wa “Yahoo” wanavyosherekea mafanikio yao/ hustle zao.

  AZONTO– inaaminika mwanzilishi wa style hii ni msanii kutoka nchini Ghana “Fuse ODG” lakini ikumbukwe awali ilikuwa ni style iliyotumiwa na makabila na iliitwa “Kpanlogo” azonto ni style nuzuri na bado vijana wanaendelea kuicheza sehemu tofauti tofauti.

  DAB– ni style mpyaaaa kabisa ambayo nchi nyingi za kiafrika zimecopy kutoka nje. nchini Nigeria ni afro hip-hop ndiyo ilipelekaea kuanza kuchezwa kwa style hiyo ya Dad, nchini Tanzania pia vijana wa kileo haiwezi kupigwa ngoma yoyote club na wimbo ukaisha bila mtu kuDab. ni style yenye mvuto wa aina yake na imetokea kupendwa na watu wengi sana.

   

  ZOMBIEWALK– wengi wanaiita style hii kama kucheza kizombi, inachezwa vizurui zaidi na wale wataalamu wa break dance ni style ambayo ni ngumu kidogo kutokana na kwamba lazima kujikunya na kunyong’oroa vizuri viungo ili kupata miondoko mizuri ya kizombi.

  Dondosha comments


  Share this