Tegemea collabo nyingine kutoka kwa Rayvanny na Diamond Platnumz

  Share this

  Ukiachana na Salome ambayo wakali kutoka WCB Wasafi Diamond Platnumz na Rayvanny wameumiza ile mbaya ipo collabo nyingine ambayo haijaachiwa ya washkaji hao wawili wameumiza tena lakini hiyo itakuwa inamilikiwa na Rayvanny.

  Amewfunguka hayo leo hii Rayvanny hitmaker wa ngoma ya Natafuta Kiki wakati akiwa kwenye interview na Dizzim Online kwenye kipindi cha Artist of the day.

  Rayvanny hakuwa tayari kufunguka ni lini itaachiwa collabo hiyo bali aliishia tu kusema wakati sahihi ukifika wa kuachiwa kwa ngoma hiyo itaachiwa.

  Saloome ni ngoma ambayo imepata mafanikio makubwa sana kwa kipindi kifupi, ikiwa ni pamoja na kulipeperusha zaidi jina la Rayvanny kimataifa hadi kumuwezesha kupata deal kadhaa kama shows na vitu kama hivyo.

  Ni matarajio ya kila mpenzi wa muziki mzuri kuwa ngoma hiyo itakuwa kali kutokana na uwezo wa kila mmoja kati yao.


  • Ukweli kuhusu ajali ya kuzama kwa Boti ya MV Burudani leo hii huko mkoani Tanga

  Dondosha comments


  Share this