Tofauti na $5000 Benpol atafanya collabo kwa makubaliano haya!

  Share this

  Mwishoni mwa mwaka jana hitmaker wa ngoma ya Moyo Mashine Ben Pol alimake headlines kwa kutweet kuwa kwa mwaka huu wa 2017 msanii yeyote atakaye muhitaji kwenye collabo ni lazima aandae kitita cha dolari elfu tano ($5000) sawa za zaidi ya shilingi million 10 za kitanzania.

  Wengi waliichukulia kitofauti kauli hiyo ukiangalia ni mtonyo mrefu kinoma ambao kautaja na kupelekea wengi kuhisi kuwa mwaka 2017 ni mwaka ambao zitasikika collabo chache kwa msanii Ben Pol.

  Perfect255 imepiga story na Ben Pol na amefunguka mengi kuhusiana na kauli yake hiyo ikiwemo na kutolea ufafanuzi ni jinsi gani ataweza kufanya collabo tofauti na pesa hiyo.

  “Ile nilimaanisha, lakini sasa kuna vitu viwili, kama msanii ana wimbo wake mzuri, na anaamini mimi nitaupenda na anaweza kunipa u miliki kwa kiasi flani katika wimbo huo anaweza kuja tukaongea, hapo tutakuwa tunaongea biashara nyingine kabisa.”

  hayo ni baadhi ya maneno ambayo Ben Pol alifunguka kuhusu ufanyaji wake collabo kwa mwaka huu wa 2017. Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumsikiliza akifunguka mwanzo hadi mwisho.


  • Roma-: Wasanii wanawekeza zaidi kwenye video kuliko Audio1 Tubadilike1

  Dondosha comments


  Share this