Tofauti na Muziki huenda tungemuona Rosa Ree kwenye upande huu

  Share this

  Huwezi kuwataja female rappers wanaofanya poa kinoma hivi sasa kwenye game ya music East Africa ukaacha kumtaja mwanadada Rosa Ree zao la The Industry, kutokana na hits ambazo anadropisha back to back, juhudi zake kwenye game na mambo mengine kibao.

  Leo Rosa Ree amekamata kipaza cha Perfect255 kutusanua kitu kingine ambacho huenda angekuwa anafanya tofauti na kuwa msanii kama ambavyo wengi tunamfahamu.

  Rosa Ree ametusanua kuwa tofauti na muziki huenda angekuwa daktari, kutokana na chaguo ambalo alikuwa amelifanya hapo awali baada ya kumaliza kidato cha sita na kuitaka familia yake iwekeze nguvu zake katika kumpa sapoti katika sekta hiyo.

  Rosa amedai kwamba alisoma kabisa masomo ya udaktari ila mwisho wa siku aliamua kuachana na harakati hizo na kuamua kufanya kile kitu ambacho anapenda (Music) na wala haikuwa shida kwa familia yake kuweza kukubaliana naye na kumpa sapoti.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili uweze kumsikiliza Rosa Ree akifunguka mwanzo mpkaka mwisho kuhusiana na mchongo huo.


   

  Dondosha comments


  Share this