TUZO 13 ZA DRAKE ZAMALIZA BIFU LA ZAIDI YA MIAKA SITA NA LUDACRIS

  Share this

  Drake ameendelea kukubali yaishe kwa wasanii wenzake ambao alikuwa hapatani nao.

  Rapper huyo ambaye ametengeneza rekodi katika tuzo za Billboard Music Awards usiku wa jana ameonyesha kuwa hana tatizo na Ludacris ambaye alikuwa mtangazaji katika tuzo hizo.

  Wakati Drake alipotajwa kwenda kuchukua tuzo yake ya ‘Top Billboard 200 Album’ alithibitisha kuwa na matatizo na msanii mwenzake huyo lakini kwa upande wake alishayamaliza na amekuwa shabiki mkubwa wa rapper huyo.

  “Ludacris, we haven’t always seen eye to eye, but I’ve always been a big fan of yours and I got a lot of love for you. I want to let you know that face to face, while I’m still here,” amesema Drizzy.

  Wawili hao waliingia kwenye bifu hilo kuanzia mwaka 2011 na tangu hapo hawajawahi kukaa pamoja.

  Dondosha comments


  Share this