Tyga na Birdman kwenye vita ya mitonyo

  Share this

  Wakati Cash Money ikiwa inadaiwa Dola Milioni 51 na Lil Wayne, Memba mwingine wa Young Money, Tyga,  ameamua kufunguka kwamba nae pia anaidai Cash Money.

  Kupitia Mahojiano yake na The Breakfast Club, Tyga alifunguka kuidai Cash Money mkwanja wa takribani dola Milioni 12 ambazo zote zinatokana na kutolipwa kwa kazi zake ambazo alizifanya kama Hooka, Molly na Rack City.

  Kitu kizuri ni kwamba Tyga ameamua kusikilizia kwanza mpaka pale Lil wayne atakapotunukiwa pesa zake ndipo nayeye aanze kufuaatilia malipo kutoka kwenye lebo hiyo ambayo inaongozwa na Birdman.

  Upande mwingine wa shilingi, Bird Man amefunguka kwa kusema kwamba Cash Money haina deni lolote kutoka kwa Tyga kwa kile kinachotajwa kwamba jamaa aliondoka kwenye lebo hiyo muda mrefu na alikuwa bado anadaiwa album moja.

  Dondosha comments


  Share this