U-Heard-: Alichokisema Fid Q kuhusu picha za Utupu za Benpol

  Share this

  Kwenye mtandao wa Instagram, kama umemfollow msanii wa Bongo fleva Benpol naamini kuanzia jana utakuwa umekutana na picha za tofauti ambazo zinapostiwa kwenye page ya mkali huyo.

  Picha ambazo zinamuonyesha Benpol akiwa katika mazingira ya utekwaji na kibaya zaidi akiwa mtupu.

  Benpol
  Benpol

  Wengi waliokutana na picha hizo wamekuwa na mapokezi ya tofauti na kuanza kudai kuwa Benpol huenda anatafuta kiki ya kuachia ngoma mpya na vitu kama hivyo.

  Kutokana na kauli ya Benpol aliyowahi kuongea kwenye XXL kuwa kila akitaka kutoa ngoma ni lazima apate wazo kutoka kwa Fid Q, kauli hiyo imemfanya Soudy Brown amvutie waya FId Q na kumuuliza kuhusu  picha hizo, huenda ikawa ni project mpya.

  Fid Q ameeleza kutoelewa chochote juu ya picha hizo za Benpol na kudai kuwa hawezi kumlaumu kwa chochote kwakuwa bado hajajua lengo hasa la yeye kufanya hivyo.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini uweze kusikiliza mazungumzo ya Fid Q na Soudy Brown kuhusu picha hizo za Benpol.


   

  Dondosha comments


  Share this