U-Heard: Chege avuta jiko kimya kimya

  Share this

  Leo kwenye XXL ya Clouds fm Soudy Brown amekuja na story anayodai kuwa amepenyezewa na Shilawadu kumuhusu mkali wa Bongo fleva Chege Chigunda, story ambayo inadai kuwa Chege yuko katika dimbwi zito la mapenzi na mrembo anayefahamika kwa jina la Zahra.

  Shilawadu wameenda mbali zaidi na kumpenyezea Soudy Brown kuwa huenda Chege Chigunda amevuta jiko kimya kimya kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ili aweze kuhalalisha suala zima la mahaba na mrembo huyo.

  Soudy Brown amemvutia waya Chege na kupiga naye story kuhusiana na tetesi hizo, ila majibu ya Chege ndio ambayo yatakuacha kinywa wazi.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili uweze kusikiliza mazungumzo ya Chege na Soudy Brown.

  Dondosha comments


  Share this