U-Heard-: Quick Rocker na Producer Luffa kwenye BIFU ZITO!

  Share this

  Producer Luffa amewasilisha malalamiko yake kwa Gossip Cop Soudy Brown baada ya kuona anachotendewa sio sawa kutoka kwa mmiliki wa studio aliyokuwa akifanyia kazi zamani Switch Records Quick Rocker.

  Luffa anadai kwamba amekuwa akisikia beats zake ambazo aliziacha studio Switch Records zikitumika bila ya yeye kushirikishwa, kitu ambacho yeye binafsi kinamuumiza na ukizingatia kuna zingine alikuwa ana malengo nazo na baadhi tayari alikuwa amekwisha wapa watu wengine ili afanye nao kazi.

  Luffa amezitaja beats za ngoma kama Uongo na Umbea ya OMG na ngoma hii mpya ya Quick Rocker inayokwenda kwa jina la Watasema kama ni baadhi ya beats zake ambazo aliziacha studioni pale.

  Soudy Brown amemtafuta kwenye line Quick Rocker na kupiga naye story kuhusiana na mchongo huo wa malalamiko kutoka kwa Producer Luffa. Unataka kujua ambacho amejibu Quick!? Bonyeza play kwenye video hii hapa chini ili kuusanukia mchongo mzima.


   

  Dondosha comments


  Share this