UGOMVI WA DIAMOND NA ALIKIBA KUMBE SABABU NI HII??

  Share this

  Wahenga wanamsemo usemao Mabeberu wawili hawaishi zizi moja, ndivyo ilivyo baina ya hawa mastar hawa kutoka tasnia ya bongo fleva Diamond Plutnumz na Alikiba kutokuwa na maelewano kwa muda mrefu na chanzo kikiwa kinafichwa.

   

  Diamond leo kupitia wimbo wake alioutoa leo mtandaoni unaoenda kwa jina la Sikomi amefunguka mengi kuhusiana na mahusiano yake aliyowahi kupitia zaidi ikiwemo yale ya yeye na mlimbwende Wema Sepetu. Ambapo ameongea amevumilia mengi wakati yupo katika penzi zito la star huyo wa bongo movie.Unaambiwa kila siku alikuwa anagombana na mama ake ila alikuwa hakomi kumpenda Wema.

  Sasa alipokuja kumwaga mchele pale aliposema “wivu ndio uliomfanya agombane na marafiki zake“. Kauli hii inakuja kuondoa utata wa yale tuliokuwa hatuyajui dhidi ya ugomvi wa yeye na Kiba, hii ndio sababu kubwa ya ugomvi wao kma ulikuwa hujui maana Wema ameshawahi kutoka kimapenzi na Alikiba. Inasemekana ugomvi huu hauwezi kuisha maana sikuzote ugomvi wa mapenzi unakuwa ni mzito.

  Dondosha comments


  Share this