Ukweli kuhusu ajali ya kuzama kwa Boti mkoani Tanga

  Share this

  Kuna taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu ajali ya kuzama kwa boti mkoani Tanga.

  XXL ya Clouds FM imemtafuta kamishna msaidizi wa jeshi la polisi mkoani humo na amethibitisha ukweli wa taarifa hizo na kutolea ufafanuzi jinsi ajali hiyo ilivyotokea na ni boti gani ambayo imezama kwenye ajali hiyo.

  “Boti yenye namba za usajili MV5512 MV Burudani iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka moja ya bandari za hapa Tanga kuelekea Pemba ilizama maji majira ya saa 8 usiku katika mkondo wa maji unaojulikana kama mkondo wa Magogo kilomita chache kutoka ufukweni mwa mkoa wa Tanga.” Alisema kamishna huyo.

  Play hii video hapa chini kumsikiliza kamishna huyo akitolea ufafanuzi zaidi juu ya ajali hiyo na taratibu za uokoaji zinaendelea vipi na zilipofikia ni wapi.

  Perfect255 inatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hiyo.


   

  Dondosha comments


  Share this