Utamu mpaka Kenya, Lulu Diva ndani ya Dili nono

  Share this

  Msanii wa Bongo fleva Lulu Diva anazidi kutupatia utamu na Good newz ni kwamba Lulu diva anaweza kuingia kwenye moja ya Management kubwa kutoka pande za 254.

  Akiwa anatamba na ngoma yake ya “Utamu”, Kipaza sauti za cha Perfect255 kilimpata Lulu Diva akiwa pande za Kenya na kutusanua kwamba amepata partnership kati ya management yake pamoja na management kubwa huko Kenya ambapo ishu kubwa ya dili hilo ni kusimamia muziki wa Lulu diva pande za Kenya na Ijumaa hii ndio itakuwa siku rasmi ambapo atasaini mkataba na kutujuza mipango mingi zaidi.

  “Ni kweli nimepata dili sio kama dili watu wanavyojua, ni partnership kati ya management yangu na management kubwa ya hapo Kenya, ambao wao kazi yao ni kusimamia muziki wangu pande za Kenya kitu kizuri Ijumaa hii tutasaini mkataba na baada ya hapo nitaweka wazi mipango kuhusu hiyo management….”Alifunguka Lulu Diva.

  Dondosha comments


  Share this