Video: Disstrack ya ‘Back 2 Back’ ya Drake bado inaishi kwa Meek Mill, cheki hapa

  Share this

  Kwa muda mrefu disstrack ya Back 2 Back ya Drake imekuwa ikisumbua kichwa cha Meek Mill, ila this time Disstrack hiyo imekuwa ndio motivation yake.

  Drake

  Kupitia video ambayo inasambaa kwenye mtandao wa Instagram, inamwonyesha rapper Meek Mill akiwa anasikiliza ngoma ya “Back 2 Back” ambayo ilikuwa ni diss aliyotunukiwa na Drake ikisemekana kama kwamba alichorewa na Ghostwriter wake.

  Ukiachana na kuisikiliza hiyo ngoma ndani ya Lamborghini yake, Meek Mill ameipa caption ngoma hiyo kama “Motivaion song” kwake.

  Mzigo huo ambao uliachiwa 2015, bado ni kidonda kwa Meek Mill, kutokana na ngoma hiyo alishwahi kuiongelea mwaka jana kwamba katika Disstrack alizotunukiwa na Drake, “Back 2 Back” ndio iliyo mkuna zaidi.

  Dondosha comments


  Share this