Video: Hakutumia kilevi, hivi ndivyo tukio zima la Tiger Woods kukamatwa na polisi

  Share this

  Baada ya stori kusambaa kuwa mcheza Golf Tiger woods alikamatwa akiwa amelewa, polisi huko Frolida wameamua kuachia video clip na kuonyesha kwamba haikuwa ulevi ila alikutwa akiwa amesinzia katika usukani wa gari yake.

  Ndani ya Clip hizi, Tiger Woods anaonekana kutoa ushirikiano mzuri na polisi ila mwili wake haukuwa kwenye hali nzuri kwani alikuwa anayumba yumba pindi alipokuwa akiambiwa afuatishe kile polisi alichokuwa akikifanya, kingine ni kwamba alikuwa hata hafahamu mahala alipokutwa na polisi.

  Tiger aliendelea kufunguka kwamba hakuwa ametumia kilevi cha aina yeyote, ila ni dawa za hospitali za kupunguza maumivu ndizo zilikuwa zikimletea tabu.

   

  Dondosha comments


  Share this