Video:Duuhh!, Nicki Minaj afunguka kulala kwa Nas ila No Kwichi Kwichi

  Share this

  Nicki Minaj aamua kuifunga stori ya kudate na Nas na kuendelea kuacha maswali kwa mashabiki baada ya kusema kwamba ameshawahi kulala nyumbani kwa Nas ila malavidavi hayakuwepo.

  Stori za Nicki na Nas zilianza muda kidogo, ila picha aliyoposti Nicki kwenye kurasa yake ndio iliyoanza kuchochea kukua kwa stori yake kuwa kwamba anatoka kimapenzi na rapper Nas, kupitia mahojiano yake aliyoyafanya na Ellen, Nicki alifunguka kwa kusema kwamba “Nas ni mfalme wa malkia, nayeye ni Queen of Queens, nina muheshimu sana na anavutia”

  Nicki Minaj aliendelea kufunguka kwa kusema kwamba huwa anaendaga kulala nyumbani kwa Nas, ila Nas hajawahi kulala kwa Nicki Minaj, kingine kikubwa ni kwamba Nicki Minaj akaongeza kwamba yeye na Nas hawajawahi kufanya mapenzi sababu kubwa ikiwa ni kwamba alipanga mwaka huu kuumaliza bila kuwa na mahusiano na mwanaume yeyote yule ila kwa upande wa Nas anaweza akamfikiria.

  Dondosha comments


  Share this