VideoFupi: Tazama marafiki wa Ivan walivyomwaga Pesa kwenye kaburi la Ivan

  Share this

  Jana May 30 ndio ilikuwa siku rasmi ya kupumzishwa kwa mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda Ivan Semwanga ambaye aliwahi kuwa mapenzini na baby mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady na kufanikiwa kupata watoto watatu, ambaye amefariki May 25 huko ncini South Africa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni shinikizo la damu.

  Mwili wa Ivan ulipumzishwa mapema hapo jana katika wilaya ya Kayunga jijini Kampala nchini Uganda ikiwa ndio nyumbani kwa wazazi wa Ivan Semwanga.

  Mengi yalijiri katika msiba huo ila kubwa zaidi ni hili la marafiki wa marehemu Ivan kumwaga pesa katika kaburi la marehemu ikiwa kama heshima kwa marehemu huyo.

  Inasemekkana ni zaidi ya shilingi za kitanzania Million 15 ambazo zilimwagwa katika kaburi hilo ikidaiwa kuwa kawaida ya vijana hao maarufu kama Rich Gang kufanya vitendo kama hivyo katika matukio mbali mbali.

  Nimeikamata video fupi ikiwaonyesha vijana hao wa Rich Gang wakimwaga pesa hizo kwenye kaburi la Ivan, bonyeza play kwenye video hii uweze kutazama.

  Dondosha comments


  Share this