Wadukuzi waendelea kumtesa Shilole

  Share this

  Ikiwa ni wiki kadhaa nyuma iliporipotiwa taarifa ya mkali wa muziki wa Bongo fleva Sholole kudukuliwa account yake ya Instagram na kumfanya mkali huyo kutokuwepo katika mtandao huo kwa takriban mwezi mmoja na kidogo, siku chache zilizopita alitutangazia kuipata account yake hiyo yenye zaidi ya followers million 2 na laki 5.

  Ila imeonekana kuwa bado account hiyo haijawa riziki kwa mwanadada huyo kutokana na kuwa bado wadukuzi hao wanaendelea kudeal na page hiyo mara kwa mara kitu ambacho kinaonekana kumkosesha raha Shilole.

  SHilole anadai kuwa account hiyo inamsaidia kutangaza biashara zake kama chakula ambacho anauza kwenye mgahawa wake na hata kazi zake za kimuziki.

  Pia Shilole amedai kuwa kudukuliwa kwa account yake hiyo ni moja kati ya sababu kubwa ambazo zimemfanya achukue muda mrefu bila kutoa ngoma mpya kutokana na kuwa anashindwa kufanya matangazo kwa mashabiki zake.


   

  Dondosha comments


  Share this