Wizkid amtia ndimu Cassper Nyovest, anatamani siku moja litokee hili

  Share this

  Muziki wa Wizkid na hatua ambayo anaipiga kila siku, imemfanya rapper kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest kutamani kuona HipHop ya Afrika Kusini kupiga hatua kama za Wizkid.

  Akiwa anatamba na ngoma kama “Tito Mbooweni” na “My dad is the superman”, Cassper ameamua kuonyesha hisia zake juu ya Wizkid na kusema kwamba anamuinspire sana kwa kile ambacho anakifanya na kutamani kuona HipHop ya Afrika kusini ipige hatua kama ya Wizkid.

  Wizkid hakukaa kimya nae akaamua kufunguka ya kwake kuhusu Cassper na kuandika kwamba “It’s all love from this side   x !!!!! Mr Fill Up! I pray we all make it  #SFTOS”

  Wizkid sasa amekuwa ni moja ya wasanii kutoka Afrika ambao ameungana na wsani kibao kutoka nje katika kupiga matamasha makubwa na kingine kizuri ni kwamba rapper Future ameamua kumchukua Wizkid katika Tour yake.

  Dondosha comments


  Share this