Video: XXL Tour Jiwe la Mwezi Arusha Episode 1

  Share this

  Mpango mzima ulianza mwezi january mwaka huu ambapo bless za kutosha zilidondokea mkoani Kigoma kwa kuweza kufungua rasmi mchongo wa Jiwe la Mwezi ambapo Darassa CMG ndio msanii ambaye aliumiza pande hizo na ngoma yake ya Muziki.

  Moshi ilifuata mwezi February na mkali kutoka Usafini WCB Richard Martin a.k.a Rich Mavoko akaumiza na ngoma yake ya Kokoro huku mwezi March Dodoma ikahusika, Moyo Sukuma Damu ya Ditto ikasimama kama Jiwe la Mwezi. April Mwanza ndio ilikuwa blessed na Phone ya Benpol ndio ilisimama huku mwezi May Wanambeya wakampokea Billnass na ngoma yake ya Mazoea.

  Historia ikaandikwa mwezi June baada ya Rich Mavoko kuumiza tena kwenye mpango wa Jiwe la Mwezi baada ya Ngoma ya Show Me ambayo amefanya na Harmonize kukidhi vigezo na kuibuka jiwe la mwezi June.

  Nakupa fursa ya kutazama intro to outro kilivyohappen pande za A Town kwenye XXL Tour ambapo Team nzima ya XXL ilikuwa imeambatana na wakali kutoka WCB Wasafi Rich Mavoko na Harmonize.

  Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kutazama Episode One kisha usicheze mbali na Perfect255 kwa muendelezo mpaka tour ilivyomalizika.


   

  Dondosha comments


  Share this