Young Killer kuja na wimbo wa kuisifia Yanga

Share this

Mkali wa muziki wa Hipohop hapa nchini Young Killer amefunguka kuwa mashabiki zake wakae tayari kuipokea ngoma yake ambayo humo ndani atakuwa anaimba na kuisifia club ya soka hapa nchini Yanga.

Ikiwa inafahamika fika kuwa rapper huyo ni shabiki wa damu wa club hiyo, amefikia maamuzi hayo baada ya kudai kuwa msimu uliopita aliitabiria club hiyo ubingwa kitu ambacho kimetokea kweli. Ikiwa katika ngoma yake ya Sinaga Swagga alisikika akisema “Mwambieni Simba kuwa Yanga ndio Mabinga na kauli ya kujipanga siku zote ni dalili ya kushindwa.”

Young Killer amefunguka hayo usiku wa jana alipoalikwa kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds fm kama mgeni rasmi na kuzungumzia mambo ya kimichezo.


 

Dondosha comments


Share this