Zari ni maana halisi ya Strong Woman-: Lulu

  Share this

  Hakuna asiyetambua ugumu ambao anaupitia Zari The Boss Lady kwasasa, ikiwa ni pamoja na kufiwa na aliyekuwa mwanaume wake ambaye walifanikiwa kupata naye watoto watatu, Ivan Semwanga almaarufu kama Ivan Don.

  Lakini bado mwanamama huyo ameonekana kusimama imara na kucheza vyema nafasi yake kama mama bora kwa watoto wa marehemu Ivan Don ikiwa inaeleweka fika hivi sasa Zari yuko mapenzini na mtanzania na Diamond Platnumz ambaye tayari wana watoto wawili.

  Muigizaji maarufu nchini Elizabeth Michael almaaruf kama Lulu ameshindwa kuficha hisia zake kwa mwanamama huyo na kuamua kuandika yakwake ya moyoni kupitia page yake ya Snapchat ikiwa ni pamoja na kumtia moyo mwanamama huyo kwa yote ambayo anayapitia katika kipindi hiki kigumu.

  Kupitia Snapchat, Lulu aliandika “Ikitokea Nimeambiwa nielezee maana ya MWANAMKE jasiri Huyu Dada atakuwa Maelezo yangu,Kwa Tuliopitia Misukosuko Tunakuelewa, Tunakuombea na kupitia hili Utaendelea Kudhihirisha Utofauti uliowekwa Ndani Yako.”

  Post ya lulu kwenye Snapchat

   

  Dondosha comments


  Share this