BOMOA BOMOA SINZA YASABABISHA HASARA KUBWA KATIKA DUKA LA AFRICAN BOY STORE

Share this

Msanii wa Bongo Flava, Jux amethibitisha taarifa za duka lake la nguo lililopo Sinza Dar es Salaam kuvunjwa.

Image result for bomoa bomoa sinza

 

Muimbaji huyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa asubuhi ya leo ndipo alipopatiwa taarifa na dada yake ambaye naye alipatia taarifa hizo na mtu mwingine, hivyo yeye akaenda kujionea kilichotokea

“Kitu kikubwa hakuna mtu aliyeumia, zimepotea pesa kidogo zilizokuwa dukani (milioni mbili) ni changamoto za maisha” amesema Jux.

Image result for bomoa bomoa sinza

“Lakini mimi ni mfanyabisha, kwa hiyo pole kwa usumbufu kwa watu wangu, kitu ambacho unaweza ukachukua ukanirudisha nyuma ni roho yangu, am hustler, siku tatu zinazokuja nafungua duka lingine African Boy store, tunahama pale hivyo ni vitu vinavyotokea kwenye maisha  na kazi nyingine zinaendelea,” ameongeza.

Image result for bomoa bomoa sinza

Jux kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Utaniua’ ambayo hadi sasa imepata views 552, 064 ndani ya siku tano katika mtandao wa YouTube kitu ambacho ameeleza hakijawahi kutokea katika ngoma zake za awali.

Dondosha comments


Share this