SIMULIZI: SINA KOSA (SEHEMU YA 2)

Share this

Sehemu ya kwanza inaishia pale ambapo konda alisita kisha akasema”nina wasiwasi na kiumbe kile uenda si kumbe wa kawaida maana miguu yake alipokua akishuka kama kwato si kwato”, 

Kwato!!!!!!, walisema kwa pamoja watu waliokua ndani ya daladala kisha konda akajibu,
” ndiyo, lakini tuachane na hayo labda sijaona vizuri jamani”, konda alimaliza na kuwaachia maswali mengi abiria.

SASA ENDELEA

Evah hakuwa na chakusema alibaki akijiwazia moyoni, Sasa kwato kwangu mimi nimekosea nn? Mmmh namuachia Mungu wangu.. Lakini mbona SINA KOSA lolote nililofanya mimi.

Aliachana na mawazo hayo kituo kilichofuata na yeye alishuka.
Alipokua akishuka alihisi maumivu kias mguuni, aliyapuuza kisha akatembea kwa kuchechemea hadi nyumbani kwake. Akaingia ndani nakujitupa katika sofa lililokuwepo sebuleni kwake, alipoketi alianza kuona tofaut katika mguu wake, taratibu mguu wake ulianza kuvimba, Evah alianza kutawaliwa na hofu moyon mwake. Kadri muda ulivyozidi kwenda mguu nao ulipata moto hali hii ilianza kumtisha Evah.

Taratiibu machozi yalianza kumdondoka Evah, machoz yalizid yakifuatiwa na kilio cha kwikwi. Maskini mguu ule ulikua ukivimba huku ukiambatana na maumivu makali Evah alianza kulia kwa sauti ya juu, kilio kile kilimshtua jirani yake aliyekua akiishi chumba cha pili, alikimbia haraka kuelekea kwa Evah,

“Evah vp tna jirani yangu mbna unalia kuna nini?” jirani aliuliza… Evah alizidi kulia huku akinyoosha kidole kuelekea mguuni kwake hali iliyomfanya jiran apige magoti kuona mguu una nini,,, “mmmh Evah umeufanya nini tena huu mguu jamani mbona unavimba na kuweka rangi nyeusi vidoleni”…

“mimi pia nashangaa ndugu yangu kuna mtu kanikanyaga kwenye gari ndo ukawa hivi” alijibu Evah… “Looh!! Uyo aliyekukanyaga sijui alivaa kiatu cha aina gani? Ngoja nichemshe maji nikukande, bila shaka hali itakua nzuri” alimaliza jirani

Baada ya muda maji yalikua tayari alimkanda jirani yake lakini badala ya kupata nafuu kila alipomkanda hali ilikua mbaya zaidi, Evah alililia kwa uchungu jamani mguu wangu nimekosa nini mimi? Mbna maumivu makali kiasi hiki Mungu wangu.Alilia bila kupata majibu jirani sasa ndiye alipata kibarua cha kumbembeleza jirani yake.. Chukua simu umpigie wifi yangu labda twende hospitali alisema Evah kwa maumivu

Machozi yalimtiririka Evah kama kamwagiwa maji sura ya huzuni aliyokua nayo ndo ilionyesha kama ni machozi.

Jirani alifanya kama alivyoagizwa na Evah alichukua simu na kumpigia wifi yake na Evah.. “hello mimi jirani yake na Evah naomba fanya haraka uje hapa unapoishi Evah ili tumpeleke hospitali maana ana hali mbaya sana” haraka jirani alitoa maelezo yaliyojitosheleza.. Wifi hakuchelewa alinyanyuka na kuelekea alikokua aliishi Evah kwani hapakua mbali sana, ilimchukua kama dakika ishirini tayari alishafika nyumbani kwa Evah alipoingia ndani alimkuta Evah amelala chini akilia “mguu wangu, mguu wangu mimi” baada ya wifi kuutazama mguu wa Evah alijikuta machozi yalimtoka pia,. Wifi huu si mda wa kulia cha kufanya tumuwahishe mgonjwa hospitali.. Alisema jirani kwa haraka wifi alijifuta machozi kisha alitoka nje na kuelekea zinapopaki taxi,, alitembea haraka haraka mpaka watu waliokua njiani walishangaa maana alikua peku, alifanikiwa kupata taxi wakawahi nyumbani kwaajili ya kumbeba mgonjwa.. Walimbeba Evah had hospitali baada ya kupokelewa walikutana na daktari ambaye alianza kuukagua mguu wa Evah, “usiwe na shaka binti una uvimbe wa kawaida tu ngoja nifanye utaratibu tukupatie tiba”aliongea dokta lakini kauli yake haikumfanya Evah apunguze kulia maana alisikia maumivu makali sana lakini kwa upande mwingine ilimpa moyo wifi ambaye alianza kupata matumaini.
Dokta alimuita nesi na kumpa maelekezo ya nini cha kufanya na dawa za kumpa mgonjwa, muuguzi aliitikia na kazi ilianza mara 1

Nesi alimpasua sehemu kidogo ya uvimbe na kisha akaanza kumkamua, lakini kadiri alivyokamua alipata mshangao “mmh huu mguu una nini badala ya kutoka usaha yanatoka meusi kiasi hiki tena mengi”alijisemea nesi kimoyomoyo alipokua akisema hayo mguu ulikua ukirudi katika hali ya kawaida taratibu wakati huo Evah alikua kwenye usingizi mzito baada ya upasuaj huo nesi alimwita wifi… “dada”.. “abee nesi”aliitika wifi na kuelekea alikolazwa Evah..

Alipofika alishangaa kumkuta wifi yake akiwa amelala na mguu uko sawa kama sio ule uliokuwa umevimba mda mfupi uliopita.. “dada nimefanya kazi hii mda mrefu lakini sijawahi kukutana
na nilichokiona leo, njoo uone kwanza” nesi yule alimwita wifi nakumuonyesha uchafu uliojaa kwenye dishi uliotoka mguuni kwa Evah.. “umechanganya na maji machafu” aliuliza wifi aliyejibiwa na nesi kwamba ulikua ni uchafu uliotoka mguuni kwa Evah.. “tuachane na hayo kwa sasa mgonjwa wenu kalala lakini akiamka ntawaruhusu pia ntawapatia dawa za maumivu ili kumuweka sawa”nesi alimaliza, wifi aliitikia kwa kichwa akiwa bado anashangaa uchafu ule.

Baada ya muda mfupi Evah aliamka akiwa mzima kabisa kisha wakaruhusiwa na kuanza kuelekea nyumbani.
Njiani Evah alitembea mzima kabisa kama si yeye aliyekuwa hoi analia mda mfupi uliopita “duu Yule kijana aliyenikanyaga ni hatari maana sio kwa maumivu yale nlokua nayasikia” alisema Evah huku anatabasamu lakini wifi hakujibu kitu alikua bado anatafakari uchafu uliotoka mguuni kwa Evah

Baada ya muda walifika nyumbani, Evah alifikia kwenye sofa wifi akapitiliza jikoni,, “ngoja niandae chakula maana nimekimbia hadi njaa ” alisema wifi na wote wakaangua kicheko.. Wakati wifi yuko jikoni ghafla alisikia miguno toka sebuleni… “tatzo lako wifi yangu hujawahi kuwa serious, umepona sasa umeanza kuniigizia, hah niache basi nipumzke kidogo maana umenikimbiza leo “alisema wifi akijua Evah anafanya utani…

“mama mama nakufaaa safari hii Evah alipiga kelele kwa nguvu zaidi maumivu yalikua mara mbili ya aliyoyasikia mwanzo na mguu ulivimba sanaa na kua mweusi sanaa”

SEHEMU YA 3 ITAENDELEAAAA… TUKUTANE JUMATANO MUDA NA WAKATI KAMA HUU.

USISAHAU KUSHARE

Dondosha comments


Share this