ufahamu mlima mrefu kuliko yote duniani

Share this

Mlima Everest ni mlima mrefu na mkubwa kuliko yote duniani wenye kimo cha mita 8,848 juu ya usawa wa bahari. mlima Everest ni sehemu ya safu ya mlima Himalaya ambapo kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na china (Tibet)

Watu wa kwanza wa kufika kwenye kilele walikuwa Edmund Hillary wa New Zealand na Sherpa Tenzing Norgay wa Nepal tarehe 29 mei 1953.

Wenyeji upande wa Nepal huuita mlima “Sagarmatha” (सगरमाथा, Mungu mama wa anga) na majirani upande wa Tibet huuita “Qomolangma” (“Mama wa dunia”).

wazungu waliokuwa wa kwanza wa kuchora ramani ya sehemu zile wakauita mwaka 1852 “Mlima XV“. Jina la Everest lilianza kutumiwa na waingereza tangu mwaka 1865 kwa heshima ya Sir George Everest aliyekuwa mpimaji mkuu wa ramani wa Uingereza kwa sababu alikuwa ameonyesha bidii kubwa katika upimaji wa Uhindi wa Uingereza (kipindi cha historia ambapo nchi za bara la hindi zilitawaliwa na Uingereza moja kwa moja ama zilikuwa chini ya usimamizi wa Uingereza)

Ramani

 

LIST YA MILIMA 10 MIREFU DUNIANI
NAMBA
JINA LA MLIMA
MITA
HATUA ZA MIGUU
MAHALI ULIPO
1.
Mlima Everest
8848
29029
Mpakani mwa Nepal na Tibet (China)
2.
K2
8611
28251
Mpakani mwa Pakistan na China
3.
Kangchenjunga
8586
28169
Mpakani mwa Nepal na India
4.
Lhotse
8516
27940
Mpakani mwa Nepal na Tibet (China)
5.
Makalu
8485
27838
Mpakani mwa Nepal na Tibet (China)
6.
Cho Oyu
8188
26864
Mpakani mwa Nepal na Tibet (China)
7.
Dhaulagiri
8167
26795
Nepal
8.
Manaslu
8163
26781
Nepal
9.
Nanga Parbat
8126
26660
Pakistan
10.
Annapurna
8091
26545
Nepal

 

 

Dondosha comments


Share this