HILI NDIO PIGO ALILOPATA DJ KHALED KATIKA ALBAM YAKE MPYA YA GRATEFUL

Share this

Baada ya kukaa kwa muda mrefu kwenye nafasi ya kwanza katika chart za billboard albamu ya mkali Dj Khaled ambayo ameipa jina la ‘Grateful’ imeshuka katika chati 200 za Billboard, huku nafasi yake ikichukuliwa na kundi la Brand New kupitia albamu yao ya ‘New Science Fiction.

Image result for GRATEFUL DJ KHALED

 

Kwa mujibu wa chati za 200 Billboard zinaonyesha kuwa albamu ya rapper huyo imeshika nafasi ya saba wakati awali ilikuwa ikishikiria nafasi ya kwanza  kwa wiki mbili mfululizo mwezi Julai,Grateful ni albamu ya 10 kwa maisha ya muziki kwa msanii huyo ambayo iliingia sokoni Juni 23 mwaka huu na tayari imeshaonyesha mafanikio mbalimbali kupitia ngoma zake 23 tofauti.

Hizi ni albamu kumi za juu katika chati za Billboard 200:-

1. Science Fiction – Brand New
2.Project Baby Two – Kodak Black
3. DAMN. – Kendrick Lamar
4.The Peace And The Panic – Neck Deep
5. Rainbow – Kesha
6. American Teen – Khalid
7. Grateful – DJ Khaled
8. Divide – Ed Sheeran
9. Paranoia: A True Story – Dave East
10. Evolve- Imagine Dragons

Dondosha comments


Share this