KUWA WA KWANZA KUIPATA ALBAM MPYA YA BEN POL YENYE NYIMBO 15

Share this

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul ‘Ben Pol ‘  ameamua kuachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol’ itakayoanza kuwa mtaani Septemba 8, mwaka huu ikiwa ni siku yake maalumu ya kuzaliwa.

Related image
Mkali huyo wa RnB Septemba 8 atasheherekea siku yake ya kuzaliwa huku akichia albamu hiyo, ambayo itakuwa ikimfikisha miaka 8 katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini,
Akizungumzia ujio wa albamu hiyo pamoja na wimbo wake mpya unaitwa ‘Kidume’ ambao amemshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Chidinma, alisema kuwa uamuzi wake wa kutoa albam ni kutaka kuendelea kuwa karibu na mashabiki wake ambao bila yao asingefika alipo.

Image result for ben pol ft chidinma
Alisema albamu mpya inatolewa rasmi kesho ambayo ni siku yake ya kuzaliwa itakuwa na  nyimbo 15, ikiwa na mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya kwa kushirikiana na wasanii wenzake wa muziki huo.
Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu sasa ni mwaka wake wa nane katika safari yake ya muziki ikiwa ni pamoja na kuungana na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimuunga mkono kila anapotoa nyimbo zake mpya.

Dondosha comments


Share this