MUSIC:HII NDIO NGOMA AMBAYO THE GAME AMEMCHANA ALIYEMUUA TUPAC NOMAA SIKILIZA HAPA

Share this

Mwaka 1996 mwezi wa 9 tarehe 13 Tupac Shakur alifariki dunia na imepita sasa miaka 21 tangu kifo chake kitokee,lakini bado msanii huyo mwenye heshima kubwa katika muziki wa HipHop nchini marekani atakumbukwa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kurap pamoja na uandishi mzuri.

eOne

Tupac pia amekuwa kama nguzo ya mziki wa HipHop nchini Marekani baada ya kuwa mtetezi wa watu weusi akitumia mashairi mbalimbali kwenye nyimbo zake ili kufikisha ujumbe kwa wale ambao walionekana kuwatenga wamarekani weusi,Ukiachana na hilo Tupac alikuwa kwenye bifu zito na hasimu wake BIG baada ya kuwepo na makundi kama East coast na Weast coat,hivyo basi kufanya mziki wa hip hop kuwana ushindani mkubwa wakati wa uhai wake.

Kizuri kutoka kwa wasanii wa Marekani ni kwamba ifikapo siku ya kumbukumbu ya kifo cha msanii huyo hufanya mabmbo mbalimbali ikiwepo kutoa nyimbo za kukumbuka harakati za msanii huyo lakini pia baadhi ya nyimbo zake hupigwa na ile studio ambayo tupac alikuwa chini yao huwa wanatoa baadhi ya ngoma ambazo amerekodi kabla ya kifo,Sasa katika kulifanikisha hilo msanii The Game ameachia ngoma yake mpya kwa ajili ya kumuenzi mkali huyo wa hiphop.

Image result for the game

The Game ameipa nyimbo hiyo jina la Heaven 4 a Gangster, nyimbo hiyo imekuwa rasmi kwa yule ambaye alimuua Tupac lakini ndani ya nyimbo hiyo ameelezea endapo tupac angekuwepo pkala leo mwaka 2017. sikiliza ngoma hapa

 

Dondosha comments


Share this