ARSENE WENGER AWEKA WAZI NI KWANINI HAKUSAINI MKATABA MPYA

Share this

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ”alisita” wakati wa kutia saini mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita kwa sababu hakuwa na uhakika kwamba ”angeweza kuiongoza klabu hiyo.”

Wenger alikubali mkataba wa miaka miwili mwezi Mei, mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika,Kwenye runinga moja nchini Ufaransa ya Telefoot, alisema alikuwa na ”sababu za kibinafsi” kutokana na uamuzi uliochelewa wa kuongeza muda wake wa miaka 21 na klabu hiyo.

Arsenal ilimaliza katika nafasi ya tano katika Ligi ya Premia msimu uliopita, ikiwa ni mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nambari nne tangu Wenger alipojiunga na klabu hiyo mwaka 1996.Hata hivyo walifanikiwa kuichapa Chelsea na kushinda kombe la FA.

Image result for arsene wenger

Arsenal walianza michuano ya msimu huu ya Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa nyumbani wa magoli 4-3 dhidi ya Leicester, kabla kupoteza kwa Stoke kwa goli 1-0 na Liverpool 4-0.”Nimekuwa na Arsenal kwa miaka mingi na msimu uliopita tulijikakamua vilivyo Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67 amesemaMwaka huu tumeshinda mechi yetu ya kwanza lakini katika mechi ya pili hatukucheza vizuri na tukapata matokeo mabaya lakini kwa hivi sasa tunastahili kujinusuru kama kawaida wakati wa shida, tunastahili kushinda mechi yetu ijayo.”

Wenger pia aliulizwa, kuhusiana na aliyoyafanya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Monaco, 21, Thomas Lemar.

Ada iliyoripotiwa na kukubaliwa ilikuwa £90m, lakini Wenger alisema kwamba mchezaji huyo ”aliamua kusalia Monaco”Aliulizwa iwapo ana mipango ya kurudi kumtafuta Mfaransa huyo wa kimataifa, Wenger amesema : ”Ndio. Kwa maoni yangu ni mchezaji wa kiwango cha juu.”

Image result for arsenal

Pia aliulizwa iwapo alitaka kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, aliyejiunga na Paris St. Germain kwa mkopo na uhamisho wa kudumu wa euro milioni 180 (£165.7m) unaotarajiwa kukamilika msimu ujao.

”Kwa kweli, milioni 180 ni kiwango cha juu sana kwetu sisi, alisema Wenger, alimtaja kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18 kama ”Pele mwengine.”

sorce BBC

 

Dondosha comments


Share this