BARCELONA WAPO TAYARI KUTOA BILLIONI 234 KWA AJILI YA KUVUNJA NDOTO ZA PEP GURDIOLA

Share this

Baada ya kuwepo kwa tetesi za kuondoka kwa Lionel Messi huku Manchester city ikihusishwa na mpango huo sasa klabu ya Fc Barcelona imeamua kumbakiza kundini mshambuliaji wake nyota na mshindi mara tano wa ballon d’or Lionel Messi.
Ili kumfanya Lionel Messi abaki Fc Barcelona imeamua kutoa kitita cha pauni milioni 80 (zaidi ya Sh bilioni 234.6) kumlipa Messi kama bonus ya usajili wake.
Kama Barcelona itafanya hivyo, itakuwa imeweka rekodi ya usajili kwa mchezaji ambaye tayari yuko ndani ya klabu kulipwa kitita kikubwa hivyo cha fedha wakati wa kuongeza mkataba.
Hata hivyo imeelezwa, FC Barcelona imelazimika kutafuta mdhamini ambaye ameipa fedha hizo na yenyewe italipa kwa kumtangaza.
Imeelezwa suela hilo la mdhamini litakuwa siri hadi hapo baadaye kila kitu kitakapomalizika.
Image result for lionel messi
Gazeti la kila wiki la nchini Hispania la L’Ara limeeleza kuwa klabu hiyo imeamua kufanya hivyo kuhakikisha Messi ambaye ni kama nembo ya klabu hiyo haondoki.
Moja ya timu zilizokuwa zimeanza kumfuatilia ni Manchester City inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola.

 

Dondosha comments


Share this