CHANZO CHA MECHI YA AZAM NA SIMBA KURUDISHWA NYUMA HIKI HAPA

Share this

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kupitia msemaji wake Alfred Lucas limetangaza mabadiliko katika mchezo kati ya Simba na Yanga ambapo awali mchezo huo ulipangwa kufanyika  kesho katika uwanja wa Chamazi Complex majira ya saa 1:00 kamili,Sasa mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Chamazi complex kama kawaida lakini muda wamchezo huo utakuwa saa 10:00 jioni.

Akizungumza juu ya mabadiliko hayo Alfred Lucas amesema kuwa baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya wahusika wa uwanja na vyombo vya usalama pamoja na mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa mhe Paul Makonda wameamua kurudisha mchezo kupigwa muda wa saa 10:00 kutokana na hali ya kiusalama hasa kutokana na ndio mara ya kwanza mechi hiyo kupigwa katika uwanja huo,Hivyo basi mashabiki wa mpira wanaombwa kufika uwanjani mapema kwa ajili ya kuwahi nafasi za kukaa na kushudia mchezo kwa utulivu.

Wakati huohuo Kocha msaidizi wa Simba jackson Mayanja amesema kikosi chake kipo kwenye maandalizi mazuri na wapo tayari kwa mchezo huo huku akisisitiza kuwa wataondoka na ushindi kwasababu wachezaji wao wako vizuri,huku wakitarajia mchezaji Emmanuel Okwi pamoja na Juko Murshid kutua leo,kwa upande wake mwakilishi wa kocha wa Azam ambaye nae ni meneja wa kikosi hicho Philip Alando amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri na wamejiandaa kufanya kile ambacho mashabiki wanatarajia huku akiongeza kwa kusema kesho ni kama sherehe sana baada ya kuruhusiwa kuutumia uwanja wao wa nyumbani kwa mechi zao zote za ligi kuu.

Dondosha comments


Share this