COUTINHO AAMUA KUACHANA NA HABARI ZA KUJIUNGA NA BARCELONA ARUDI NYUMBANI BRAZILI

Share this

Brazil imeanza maandalizi ya kujiandaa na mechi yake ya kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador na kati ya wachezaji waliomo katika kikosi hicho ni Philippe Coutinho ambaye hajaanza kuichezea timu yake ya Liverpool msimu huu kwa madai kuwa ana “stresi”.
Cha kushangaza Coutinho ameonekana ni mwenye furaha sana akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil wakiwa wana jiandaa kucheza mechi yao ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Ecuador,Mchezaji huyo ambae ameonekana kuiweka kwenye wakati mgumu timu yake ya liverpool baada ya kutuma maombi ya kuihama klabu hiyo nakutaka kwenda Barcelona.
 Lakini bado timu hizo mbili hazijafikia muafaka jambo ambalo linasababisha mchezaji huyo kutoonekana katika kikosi hicho ambacho hata hivyo, kinaendelea kufanya vema katika michezo ya ligi kuu.

 

 

 

 

 

Dondosha comments


Share this