FRANK DE BOER ATUPIWA VIRAGO CRYSTAL PALACE,NAFASI YAKE YACHUKULIWA NA HUYU HAPA

Share this

KOCHA Frank de Boer amefukuzwa katika klabu ya Crystal Palace leo na nafasi yake itachukuliwa na Roy Hodgson Uwanja wa Selhurst Park,De Boer anafukuzwa kutokana na matokeo mabaya baada ya kushindwa kupata japo pointi au kufunga bao moja katika mechi nne za awali za Ligi Kuu ya England,ikiwemo ya Jumapili ambayo walifungwa na Burnley.
Mrithi wake Hodgson anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili The Eagles baada ya kumzidi kocha mwenzake wa zamani wa England Sam Allardyce ambao kwa pamoja walikuwa kwenye mbio za kuwania nafasi hiyo.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 70 anatarajiwa kurejea kwenye Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka West Brom kujiunga na timu ya taifa mwaka 2012, baada ya awali kuzifundisha Liverpool, Fulham na Blackburn katika michuano hiyo mikubwa ya klabu nchini humo.
He is expected to be replaced in the Selhurst Park dug-out by ex-England boss Roy Hodgson
Hodson amekuwa nje ya kazi tangu England ivurunde kwenye michuano ya Euro 2016 ilipotolewa na Iceland lakini mtu huyo kutoka taifa la Croydon anakwenda kufundisha klabu aliyoichezea akiwa kijana mdogo miaka ya 1960.
Kuondoka kwa De Boer pia kutamfanya na Sammy Lee aondoke klabuni hapo ambaye aliingia kwenye klabu hiyo pamoja na Allardyce huku Ray Lewington anawasili katika benchi la Ufundi la Hodgson.
De Boer hides his head in his hands during the home defeat to Swansea City last month
 MECHI ZILIZO MFUKUZISHA DE BOER
Agosti 12: v Huddersfield (nyumbani) – lost 3-0
Agosti 19: v Liverpool (ugenini) – lost 1-0
Agosti 22: v Ipswich Town (LC) – won 2-1 
Agosti 26: v Swansea (nyumbani) – lost 2-0
Sept 10: v Burnley (ugenini) – lost 1-0 
WASIFU WA KOCHA HODSON
1976–1980: Halmstad
1982: Bristol City
1982: Oddevold
1983–1984: Orebro
1985–1989: Malmö
1990–1992: Neuchâtel Xamax
1992–1995: Switzerland
1995–1997: Inter Milan  
1997–1998: Blackburn Rovers
1999: Inter Milan (caretaker) 
1999–2000: Grasshoppers 
2000–2001: Copenhagen
2001: Udinese
2002–2004: United Arab Emirates
2004–2005: Viking
2006–2007: Finland
2007–2010: Fulham
2010–2011: Liverpool
2011–2012: West Bromwich Albion
2012–2016: England 
2017: Crystal Palace 

Dondosha comments


Share this