HIKI NDICHO WALICHOKIFANYA SERENGETI BOYS DHIDI YA MALI NCHINI GABON

Share this

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imegawana pointi na mabingwa watetezi, Mali katika mchezo wa kwanza wa Kundi B Fainali za Mataifa ya Afrika jioni ya leo Uwanja wa l’Amitie Sino mjini Libreville, Gabon.
Ulikuwa mchezo mkali kama ilivyotarajiwa na Mali ndiyo walioutawala zaidi na pengine kutokana na serengeti boys kucheza kwa tahadhari ya kujihami zaidi.
Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu na kupanga vyema mashambulizi yao, lakini safu ya ulinzi ya Tanzania ilicheza vizuri na kuokoa hatari nyingi ukiacha chache ambazo mabingwa hao watetezi walipoteza wenyewe.

Image result for mali vs tanzania
Lakini sifa zaidi zimuendee kipa wa Tanzania, Ramadhani Kabwili aliyeokoa michomo mingi ya hatari ya washambuliaji mafundi wa Gabon.
Kwa kutumia mfumo wa kushambulia kwa kushitukiza, Serengeti Boys nayo ililikaribia mara kadhaa lango la Mali, lakini wakashindwa kutumia nafasi.


Na zaidi Serengeti Boys ilipata nafasi za kufunga kipindi cha pili, huku nafasi nzuri zaidi akiipoteza Assad Ally ambaye akiwa amebaki na kipa wa Mali, Alkalifa Koulibaly kwenye akapiga ovyo mpira ukapotea.
 

Dondosha comments


Share this