HUU NDIO USAJILI GHALI ULIOFANYIKA TANGU DIRISHA LA USAJILI KUFUNGULIWA

Share this

Usajili barani ulaya unaendelea kushika kasi baada ya vilabu mbalimbali kutafuta wachezaji katika vilabu mbalimbali na tangu dirisha la usajili lifunguliwe ,klabu ya Man United imeshavunja rekodi katika usajili baada ya kutumia kiasi cha pauni 75 millioni kwa ajili ya kupata huduma ya mshambuliaji Romelu Lukaku.
Wafuatao ni baadhi ya usajili uliotumia gharama kubwa tangu dirisha kufunguliwa

 

Beki Antonio Rudiger amesajiliwa na klabu ya Chelsea kutoka Roma kwa kiasi cha Pauni milioni 34.
Mjerumani huyo,24, amesaini kandarasi ya miaka mitano na mabingwa hao wa England baada ya hivi karibuni kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya ujerumani kubeba kombe la mabara nchini Rusia.Image result for rudiger to chelsea

Mshambuliaji raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Man United,akitokea katika klabu ya Everton kwa ada ya pauni millioni 75.

Image result for lukaku to manchester united

Alexandre Lacazette amesaini mkataba wa miaka 5 wa kujiunga na Arsenal. Ada ya uhamisho imevunja rekodi ya Arsenal, imelipwa kwanza €53m na huenda ikafikia €60m kulingana vipengele vya performance ya mchezaji.

Image result for lacazetteWinga wa Misri Mohamed Salah amejiunga rasmi na Liverpool akitokea AS Roma kwa ada ya uhamisho ya paundi millioni 39.

Image result for mohamed salah liverpool
Bernardo Silva amejiunga rasmi na Manchester City akitokea Monaco kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia €50m

Image result for bernardo silva

Manchester City wamekamilisha usajili wa golikipa wa Benfica Ederson Moraes kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi zote za nyuma kwa magolikipa – £45m.
Related image

Klabu ya Bournemouth imemsajili kipa Asmir Begovic kutoka Chelsea kwa ada ya pauni milioni 10

Image result for Asmir Begović
Beki wa kimataifa wa Ureno, Pepe ameipiga chini ofa ya kujiunga na Inter Milan na PSG, baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Basiktas ya Uturuki. Pepe alimaliza mkataba wake na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliomalizika.
Image result for pepe in besiktas

Baada ya kucheza La Liga kwa kipindi cha miaka 13 katika vilabu vya Espanyol na Malaga, golikipa Mcameroon Carlos Kameni amejiunga na klabu ya Fernebahce ya Uturuki.

Image result for kameni to fenerbahce

Dondosha comments


Share this