JE ?KUKOSEKANA KWA SADIO MANE NI PIGO KWA LIVERPOOL NA AHUENI KWA MAN UNITED TOA MAONI YAKO

Share this

KLABU ya Liverpool imepata pigo kufuatia habari kwamba mshambuliaji Sadio Mane ameumia nyama za paja na anatakiwa kuwa nje kwa wiki sita.
Mane, ambaye amefunga mabao matatu kwenye mechi nne za Ligi Kuu ya England hadi sasa msimu huu, alitolewa dakika ya 89 Jumamosi Senegal ikishinda 2-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mechi ya kufuzu Kombe Ia Dunia. Image result for sadio mane
Mchezo wa kwanza atakaoukosa ni wa nyumbani dhidi ya Manchester United Jumamosi. Wiki sita ambazo atakaa nje, atakosa mechi nane za Liverpool, ukiwemo wa Ligi Kuu wa nyumbani dhidi ya Chelsea.
Mane ni tegemo katika mfumo wa kocha Mjerumani, Jurgen Klopp Liverpool na kukosekana kwake ni pigo.
Liverpool inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 12 kutoka mechi zao saba za mwanzoni na wametoa sare mechi zao mbili za mwanzo za Ligi ya Mabingwa.Image result for sadio maneMchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Mane tayari amekosa mechi tatu msimu huu alipokuwa akitumikia adhabu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu kipa wa Manchester City, Ederson mwezi uliopita katika mchezo wa Ligi Kuu.
Klopp sasa atalazimika kuchagua wachezaji wengine wa kutumia kipindi hiki hadi Mane atakaporejea mwishoni mwa Novemba.
Washambuliaji Daniel Sturridge na Dominic Solanke watagombea nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, wakati Philippe Coutinho, Roberto Firmino na Mohamed Salah  wanaweza kuanzishwa pamoja pia kwenye safu ya ushambuliaji.

MECHI ZA LIVERPOOL BILA SADIO MANE

(Nyumbani) Manchester United – Oktoba 14
(Ugenini) Maribor – Oktoba 17
(Ugenini) Tottenham – Oktoba 22
(Nyumbani) Huddersfield – Oktoba 28
(Nyumbani) Maribor – Novemba 1
(Ugenini) West Ham – Novemba 4
(Nyumbani) Southampton – Novemba 18 
(Ugenini) Sevilla – Nov 21 
Liverpool watakuwa wenyeji wa Chelsea Uwanja wa Anfield Novemba 25

Dondosha comments


Share this