KITABU ALICHOKUWA ANASOMA CHRISTIANO RONALDO,CHAZUA UTATA KUELEKEA FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA.

Share this

Image result for cristiano ronaldo read bookJumanne jioni nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kupitia Akaunti yake ya Instagram alipost Picha ikimuonesha anasoma Kitabu huku akiandika “Drinking my tea and reading my book..” akimaanisha kuwa “Ninakunywa Chai Yangu na ninasoma kitabu changu,” . .

Post hiyo ilipata Comments nyingi, huku wengi wakiuliza ni kitabu gani Mreno huyo alichokuwa anakisoma kuelekea mchezo wa fainali klabu bingwa Ulaya..? .

Kitabu hicho kilichokuwa mikononi mwake kinaitwa (O Sucesso Nao ocurre por acaso ) .
(Success Is No Accident), kikimaanisha kuwa Mafanikio Si Ajali koitabu hiko kimeandikwa na Doctor Lair Ribeiro, kina kurasa 127.

Kitabu hiki kinaelezea kuwa hakuna kitu kinatokea kwa bahati (Ajali) katika maisha, fursa hutokea kila wakati, lakini unatakiwa kujiandaa kuzitumia vyema.

Mwandishi wa kitabu hiko anasema kwamba “Nafasi na bahati havipo kabisa” na kinaonesha kuwa ” Kuna watu ambao wanamafanikio katika kipindi chao chote cha maisha na wengine ambao wanatumia maisha yao kupambana kupata yale mafanikio wanayoyataka”.

Kimsingi ni kitabu kizuri kinachofundisha jinsi gani ya kunufaika na hali ili kuleta mafanikio katika maisha.


Dr. Lair Ribeiro anapendekeza kwa kusema  ” Sisi ni nguvu ya Ubunifu wa maisha yetu na tunaweza kuandika Stori zetu zenye mafanikio,Kushinda vile tunavihitaji kweli kwa kuamini kuwa tunaweza kupata kila kitu tunachokiota “.

Dondosha comments


Share this