KUMBE DYBALA NDIO CHANZO CHA DANI ALVES NA LEONARDO BONUCCI KUHAMA JUVENTUS

Share this

 

Baada ya miaka 7 akiwa na Juventus, beki kisiki Leonardo Bonucci ametua katika klabu ya AC Milan kwa ada ya pauni millioni 35.
Huenda huu ukawa usajili ambao umewashtusha baadhi ya watu katika kipindi hiki cha usajili kwani kuna sababu ambazo zimeripotiwa kufanya mchezaji huyo kuondoka Juventus kwa kushtukiza.

Image result for dybala,bonucci and alves

Inaelezwa kuwa uhusiano kati ya kocha wa Juventus Massimiliano Allegri na Bonucci ulianza kuharibika baada ya mshambuliaji Paulo Dybala mwezi April mwaka huu kusaini mkataba mpya wenye thamani ya euro milioni 7 kwa mwaka wakati Bonucci anapata euro milion 3 kwa mwaka, Bonucci alisikitishwa wazi wazi na kitendo hicho na kudhihirisha kutoridhishwa na hali hiyo kwenye mazoezi na vyumba vya kubadilishia nguo.

Msimu ulivyokuwa unaendelea matatizo mengine yaliendelea kuzuka kwani Bonucci aliachwa kwenye mchezo wa 16 Bora UCL dhidi ya FC Porto kwa sababu za kinidhamu cha kushangaza zaidi ni Kipindi cha kabla ya fainali ya klabu bingwa ulaya dhidi ya Real Madrid, Dybala alikuwa anatumia simu yake kitu ambacho kinazuiliwa vikali na uongozi wa Juventus ndipo Dani Alves akaipiga simu kutoka katika mikono ya Dybala na kumwambia “ Huu si muda wa kutumia simu yako“. lakini baada ya tukio hilo Ugomvi mkubwa  kati yao ukazuka.

Related image

Kipindi cha mapumziko ya mchezo wa fainali Alves alimkosoa Dybala kwa kiwango alichoonesha katika kipindi cha kwanza na ugomvi kati yao ukazuka tena lakini wakati huu Bonucci akaingilia cha kushangaza ni pale ambapo Kocha Allegri akamtetea Dybala lakini mkongwe Bonucci akaja na kumkosoa vikali Dybala.

Image result for dybala,bonucci and alves

Siku inayofuata Allegri alienda kwa bodi ya klabu na kutamka kuwa hatasaini mkataba mpya kama Bonucci na Alves wataendelea kuwepo katika timu hiyo.
Na hizo sababu ndizo zikasababisha Alves kuondoka huru Juventus akiwa ameitumikia kwa msimu mmoja tu, Bonucci alipata ofa kutoka katika klabu za EPL, Man City na Chelsea lakini Muitalia huyo akaamua kubaki Italia kwa sababu za afya ya mwanae wa kiume

 

Dondosha comments


Share this