KWA HIKI ANACHOFANYIWA DIEGO COSTA NDANI YA CHELSEA KINAITWA KOMOA NI KUKOMOE

Share this

Bado mambo yanaonekana ayako sawa katika kile kinachoendelea kufanyika katika klabu ya Chelsea,Baad ya kuonekana katika miji ya London majaliwa ya straika Diego Costa yanazidi kuwa tata kutokana na tukio ambalo limejitokeza katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Chelsea.

Image result for diego costa arrive chelsea
Tukio zima lilikuwa hivi wafanyakazi wa Chelsea walilazimika kulitoa gari la Costa lililokuwa lime egeshwa kwenye eneo la magari ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na kulipeleka kwenye eneo la wachezaji vijana wanapoegesha magari yao hii ni kutokana na mabosi wa Chelsea kuagiza gari hilo aina ya Range Rover kuondolewa alipokuwa ameliegesha na kulihamisha kwenye ile sehemu ya kuegesha magari ya vijana ili kumfanya kutojichanganya na wenzake wanaocheza kikosi cha kwanza.

Image result for diego costa arrive chelsea

 
Costa alirejea klabuni hapo hivi karibuni baada ya kuwa nje ya England licha ya msimu kuanza kutokana na kutofautiana na kocha wake Antonio Conte,hata hivyo kutokana na tukio hilo bado inaonekana hali si shwari katika klabu hiyo,Na aijulikani ni lini Costa ataanza kufanya mazoezi ama kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo,Ikumbukwe kuwa Costa alikuwa anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.

Dondosha comments


Share this