KWA TUKIO HILI ALILOFANYA KWA REFA DELE ALLI MBIONI KUFUNGIWA NA FIFA

during the Barclays Premier League match between XXX and XXX at
Share this

Katika mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya England dhidi ya Slovakia Kiungo wa Tottenham Dele Alli amelazimika kuomba msamaha kwa kitendo chake cha kuonesha kidole cha kati kunako dk 77 ya mchezo huo hapo jana.

Image result for dele alli show middle finger

Alli alionesha ishara hiyo muda mchache baada ya kuchezewa vibaya na Martin Skrtel, na mwamuzi kuamuru mchezo uendelee,Inasemekana Alli alionyesha ishara hiyo kwa mwamuzi raia wa ufaransa Clement Turpin baada ya mwamuzi huyo kuto puliza filimbi ili kuamrisha kama ni faulo,lakini baada ya mchezo kiungo huyo alisema kuwa kutokana na kitendo yeye alikuwa akimtania mchezaji mwenzake wa England Kyle Walker (na si kwa ajili ya mwamuzi).

.
“Kwa ufafanuzi ishara ya usiku huu ilikuwa utani kati yangu na rafiki yangu kipenzi Kyle Walker ! Samahani kwa chukizo lolote nililosabisha !..” aliandika Alli katika ukurasa wake wa Twitter.

Image result for dele alli show middle finger

Lakini kama FIFA watafanya uchunguzi na kugundua kuwa kidole cha kati alicho onyesha delle alli alikuwa anamuonyeshea mwamuzi, Alli anaweza kufungiwa takribani mechi 3 ,Hata hivyo Kocha wa England Gareth Southgate amemtetea mchezaji huyo akisema kuwa wawili hao (Alli na Walker) huwa wana njia mbaya ya kufanya mawasiliano.

Dondosha comments


Share this