MAMBO MATANO MUHIMU KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI EUROPA LEAGUE AJAX NA MAN UNITED

Share this

 1:  Ajax waonyesha kuguswa na tukio la ugaidi la jijini Manchester

Ajax held a minute's silence for the Manchester terror attack victims on Tuesday afternoon

Kuelekea mchezo wa fainali ya Europa League utakao fanyika leo katika uwanja wa Friends Arena jijini Stockholm nchini Sweden kocha wa Ajax Peter Bosz ametoa pole zake kwa niaba ya uongozi na wachezaji wa timu hiyo wakati akifanya mkutano na waandishi wa habari leo huku akianza kwa kingereza na kuomba atumie lugha ya kiholanzi ili apate maneno ya dhati kabisa

Ningependa kusema kitu kwa tukio lilitokea Manchester,lakini naomba niongee kwa lugha ya kiholanzi ili nipate maneno sahihi,Aliendelea kwa kiholanzi kwa kusema Mawazo yetu Aliendelea katika Kiholanzi: “Mawazo yetu ni pamoja na waathirika na familia zao matukio ya kutisha kama haya inapaswa kutupiwa jicho pia mchezoni tunatoa pole sana kwa familia na tuna lahani vikali tukio hilo.

Katika hatua nyingine kikosi cha Ajax kimefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Friends Arena na kuonyesha heshima kwa waathirika wa tukio la manchester.

2.DOLBERG ndio mchezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo huo

Image result for kasper dolberg

Kasper Dolberg mwenye umri wa miaka 19 ndiye mchezaji hatari zaidi katika kikosi cha Ajax baada ya kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 22 katika ligi kuu ya uholanzi,kocha wa Ajax amethibitisha kwa kusema Dolberg ni kijana mdogo lakini maendeleo yake ni ya ajabu huku akiwa na umri wa miak 19 .

3.Kocha:Tutacheza mchezo wetu wa kila siku

Image result for Ajax formation 2016/2017

Kocha wa Ajax amesema watacheza mchezo wao wa kila siku bila kubadilisha kitu chochote”Tumekuwa na maendeleo katika mfumo wetu ambao tunacheza na tutatumia staili yetu ile ile nadhani itatupa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi” Pia mchezaji kiungo wa timu hiyo Lasse Schone ameongeza kwa kusema”sisi ni timu mbili tofauti na tumekutana na presha tofauti na tunatumia mifumo tofauti tunachotakiwa ni kusimamia katika kile ambacho kimetufanya kufika hapa nadhani tutapata tunacho stahili.

4. vijana hawana wasiwasi wa kupambana

Image result for ajax squad 2017

kikosi cha Ajax kimesheni vijana chipukizi na wataalam wa soka wanadhani vijana hao watakuwa na uoga wa kupambana katika mchezo wa fainali hasa baada ya timu ya Manchester united kuwa na wachezaji wengi wakubwa lakini kocha wa Ajax ametoa kauli ya kusema “vijana wake wako timamu kiakili na kimwili na hawana uoga wa kupambana katika mchezo huo” Wachezaji wa Ajax wameonekana wakijifua kwa nguvu leo asubuh kuelekea mchezo huo uku wakipiga mipira ya mbali wakati gplikipa wa zamani wa Manchester united akionekana kumpa maelezo makini kipa kinda wa cameroon na golikipa namba moja wa Ajax Andre Onana

5.Kukosekana kwa Ibrahimovic katika ardhi ya nyumbani

Image result for ibrahimovic ajax

Mshambuliaji tegemeo wa United atakosa mchezo huo wa fainali baada ya kuwa nje kwa majeraha aliyo yapata katika mchezo wa nusu fainali lakini atakuwa katika jukwaa la uwanja wa Friends Arena kuwapa sapoti wachezaji United,Lakini sio yeye tu atakaye kosekana wapo Luke shaw,Ashely young na Marcos rojo.Hata hivyo kukosekana kwa mchezajin huyo kumemfanya kocha wa Ajax kumwagia sifa mchezaji huyo kwa kusema “Ni mmoja kati ya watu wenye historia nzuri katika klabu hii ya Ajax na kwa umri wake bado anaitumikia klabu kubwa duniani ni jambo la kushangaza sana nadhani angekuwepo kwenye fainali hii kama sio majeraha nadhani tutamiss sana katika fainali”Alisema

 

Dondosha comments


Share this