Manchester United wako tayari kutoa kitita hiki kumnasa Marco Verratti

Share this

Baada ya kuinyaka saini ya Mbelgiji Romelu Lukaku, club ya Manchester United bado inaonekana ina nia thabiti ya kuendelea kukiimarisha kikosi chake kwa kuendelea kusajili wachezaji mbalimbali wanaoonekana kuwa na mantiki kwa kocha mreno Jose Mourinho.

Manchester United wametangaza utayari wao wa kuidondoshea club ya Paris Saint Germain kitita cha Pound mil 70 ili kuinasa saini ya kiungo wa club hiyo Marco Verratti.

Usiku wa kuamkia leo United imetoa sare ya bao 1-1 katika mchezo wake dhidi ya Real Madrid uliopigwqa huko nchini Marekani kwenye International Champions Cup.


 

Dondosha comments


Share this