Manny Pacquiao kukichafua upya April

Share this

Kama ulikuwa unasema kwamba Manny Pacquiao anastaafu maswala ya ngumi, anza kulifuta hilo wazo kichwani.

Baada ya kuwa na mastori kibao kuhusu kuachana na ngumi na kuweka malengo mengi zaidi kwenye maswala yake kwenye siasa, Manny Pacquiao anarudi upya ulingoni April 22 mwaka huu kupambana na Jeff Horn bondia kutoka Australia.

Licha ya kuwa bado kuna maswala ya kutafuta ukumbi kwa ajili ya pambano hilo, mapromoter wamekuwa wakichagua kwenda Australia, Us na  United Arab Emirates ambapo wanategemea kukinukisha huko.

Najua mashabiki wengi wa ndondi na hata wale ambao sio wa mchezo huo wamekuwa wakiomba leo kurudiana kwa pambano kati ya Floyd Mayweather na Manny kurudi upya ulingoni, japokuwa Mayweather ameshastaafu ila wawili hao wanasubiriwa kwa hamu zote.

 

Dondosha comments


Share this