MARIA SHARAPOVA AKUTANA NA JANGA LINGINE BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO CHA MIAKA SABA

Share this

Umekuwa msimu mbaya kwa mwanadada machachari katika mchezo wa tenisi raia wa Urusi, Maria Sharapova baada ya kutolewa nje ya  mashindano ya wazi ya Marekani (US Open) baada kukubali kipigo kutoka kwa mwanadada, Anastasija Sevastova katika mzungungo wa nne.

Image result for anastasija sevastova

 

Maria Sharapova unazidi kuwa na mwaka mbaya baada ya kukaa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja na miezi 7 amekubali kipigo cha jumla ya seti 5-7 6-4 6-2 kutoka kwa Sevastova aliyetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo huko New York,Nahiyo ndio inakuwa michuano ya kwanzaya Grand slam kwa Sharapova .

Image result for maria sharapova

Sevastova mwenye umri wa miaka 27 sasa anatarajia kukutana na mmarekani, Sloane Stephens katika hatua ya robo fainali baada ya kumfunga Julia Goerges,Baada ya mchezo Sharapova mwenye umri wa miaka 30 amesema“Ulikuwa mchezo mzuri sana wa wiki iliyopita, nimejifunza mengi na ilikuwa nafasi muhimu kwangu na shukuru sana kwa kupata nafasi hiyo”, amesema Maria Sharapova.

Dondosha comments


Share this