MASAA MAWILI TU YAMKWAMISHA PHILIPPE COUTINHO KUTUA BARCELONA

Share this

Dirisha la  usajili nchini Hispania limefunga usiku wa jana na kushuhudia baadhi ya vilabu mbali mbali vikikamilisha usajili wa wachezaji mbalimbali ili kuimarisha vikosi vyao katika msimu huu mpa wa mwa 2017/2018.

Kwa upande wa klabu ya Barcelona ambao walikuwa wanawania sahihi ya mchezaji raia wa Brazil anayechezea katika klabu ya Liverpool Phillipe Coutinho ulishindikana baada ya klabu a liverpool kukataa ofa zaidi ya nne na kusisitiza kuwa mchezaji huyo auzwi,hata hivyo mchezaji huyo alituma maombi ya kuihama lakini wamiliki wa klabu hiyo waligoma kumuuza.

Image result for PHILIPPE COUTINHO

Cha kusangaza klabu ya Liverpool ilionekana kulegeza msisitizo wa kuto muuza Coutinho baada ya jana yakiwa yamebaki masaa mawili dirisha kufungwa kutangaza ofa ambayo endapo Barcelona wangeweza kutoa basi Coutinho angeruhusiwa kuondoka Anfield,Liverpool walitangaza ofa ya pauni millioni 160 sawa na euro millioni 146 huku mchezaji huyo akitua Barcelona januari,lakini klabu ya Barcelona wao walikuwa tayari kutoa €120m (£110m) jumlisha €40m (£36m) baadae.

Wakati huo huo Angel Di maria pia alishindwa kukamilisha dili lake la kutua Barcelona baada ya PSG kutaka ada ya €80m (£73m) lakini Barcelona walishindwa kukamilisha usajili huo chini ya mkurugenzi wa michezo Robert Fernandez.

Image result for dimaria

Dondosha comments


Share this